Kocha Mkuu Pablo Franco amefanya mabadiliko ya wachezaji wanne katika kikosi kitakachoanza leo kwenye mchezo dhidi ya Geita Gold ukilinganisha na kile kilichocheza na Azam FC.
Pablo amemuanzisha mlinda mlango Beno Kakolanya walinzi Gadiel Michael na Pascal Wawa pamoja na kiungo Taddeo Lwanga.
Nahodha John Bocco ataendelea kuongoza safu ya ushambuliaji akisaidiwa na viungo washambuliaji Pape Sakho, Rally Bwalya na Kibu Denis.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Beno Kakolanya (30), Shomari Kapombe (12), Gadiel Michael (2), Joash Onyango (16), Pascal Wawa (6), Taddeo Lwanga (4), Kibu Denis (38), Sadio Kanoute (13), John Bocco (22), Rally Bwalya (8), Pape Sakho (10)
Wachezaji wa Akiba
Ally Salim (1), Jimmyson Mwanuke (21), Mohamed Hussein (15), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Peter Banda (11), Mzamiru Yassin (19), Medie Kagere (14), Yusuf Mhilu.