Wachezaji wetu wa timu ya Wanawake ya Simba Queens wamejawa na matumaini makubwa ya kushinda na kutinga nusu fainali ya michuano ya Caf Women’s Champions League Cecafa Qualifiers 2021.
Simba Queens inashuka dimbani kesho katika Uwanja wa Nyayo kuwakabili wenyeji Vihiga Queens mchezo utakaoanza saa saba mchana.
Mshambuliaji kinara Oppah Clement, amesema mchezo utakuwa mgumu na tunajua tunaenda kucheza na wenyeji lakini matumaini ya kushinda ni makubwa kutokana na maandalizi tuliyofanya.
“Tutahakikisha tunawapa furaha Wanasimba kwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa kesho ingawa utakuwa mgumu na tunaenda kucheza na wenyeji lakini tumejiandaa vizuri na matumaini ya kuibuka na ushindi ni makubwa,” amesema Oppah.
Kwa upande wake mlinzi wa kushoto, Fatuma Issa ‘Fetty Densa’ amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na morali ipo juu na matumaini ni makubwa.
Nae mlinda mlango, Zubeda Mgunda amesema kwa ubora wa kikosi tulionao na maandalizi tuliyofanya matumaini ya kushinda ni makubwa na kuingia fainali.