Kiungo mpya mshambuliaji, Said Ntibazonkiza ameanza kikosi cha kwanza kitakachoshuka dimbani leo saa 12:15 jioni kuikabili Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kocha Mkuu Juma Mgunda amempanga Saido nyuma ya mshambuaji John Bocco akicheza namba 10.
Huu utakuwa mchezo wa kwanza wa Ntibazonkiza kucheza akiwa na jezi yetu na utakuwa wa mwisho kwetu katika mwaka 2022.
Kikosi kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), John Bocco © (22), Saido Ntibazonkiza (39), Pape Sakho (10).
Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Victor Akpan (6), Jonas Mkude (20), Kibu Denis (38), Habibu Kyombo (32), Augustine Okrah (27).