Ntibazonkiza akabidhiwa tuzo yake ya Januari

Kiungo mshambuliaji, Saido Ntibazonkiza amekabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Januari (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Ntibazonkiza amewashukuru wachezaji wenzake kwa ushirikiano waliompa uwanjani, benchi la ufundi kumpa nafasi na mashabiki waliompigia kura kwa wingi.

Saido amesema amesajiliwa kwa ajili ya kuisaidia timu kufanya vizuri na amefurahi kuona msaada wake uwanjani pamoja na wenzake unafanya vizuri.

“Nimefurahi kupata tuzo hii, ina maana kubwa kwangu. Nawashukuru familia yangu, wachezaji, benchi la ufundi pamoja na mashabiki kwa ushirikiano huu mkubwa.

“Pia nawashukuru wadhamini Emirate Aluminium Profile kwa kutuandalia tuzo hii, bahati nzuri naifahamu Emirate maana hata kwetu Burundi ipo. Inatuongezea morali wa kuipambania timu siku zote,” amesema Saido.

Katika mwezi Januari, Saido amecheza mechi tatu sawa na dakika 270 akifunga mabao mawili na kusaidia kupatikana kwa lingine moja.

Saido amekabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile kama sehemu ya zawadi ya kuibuka mshindi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER