Ni ama zao ama zetu kwa Mkapa leo

‘Ama Zao Ama Zetu’ ndiyo kauli pekee unayoweza kuitumia kuelezea mchezo wetu wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs leo utakaopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Katika mchezo wa leo tunahitaji kupata ushindi, tena si ushindi wowote bali wa mabao 5-0 ili kutinga moja kwa moja Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika au mabao 4-0 ambayo yatatupeleka katika muda wa ziada.

Ingawa kiuhalisia si kazi rahisi kufanikisha hilo lakini kuanzia uongozi, benchi ya ufundi, wachezaji hadi mashabiki tuko pamoja na tunaamini tunaweza kupindua matokeo na kutinga nusu fainali.

Baada ya kikosi kurejea kutoka Afrika Kusini, Jumanne kilianza maandalizi moja kwa moja ya mchezo wa leo huku kila mchezaji akihakikisha anatimiza majukumu yake ipasavyo.

KAULI YA KOCHA GOMES

Kocha Mkuu Didier Gomes amesema kwenye mpira kila kitu kinawezekana na tumejitahidi kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo uliopita na kama tukipambana kiume tunaweza kupindua matokeo na kutinga nusu fainali.

“Tunajua tuna kazi kubwa ya kufanya, lakini kwenye mpira kila kitu kinawezekana. Wachezaji wapo kwenye hali nzuri na kila mmoja anatamani ajumuishwe kikosini lengo ni kupindua matokeo na kuweka rekodi barani Afrika,” amesema Gomes.

TAARIFA YA KIKOSI

Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo isipokuwa tutakosa huduma ya kiungo Jonas Mkude ambaye ana matatizo ya kifamilia.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER