Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ amemkabidhi kitita cha Sh. 5,000,000 nahodha John Bocco baada ya ushindi wa bao moja tulilopata dhidi ya Vipers.
Pesa hiyo ni zawadi ya hamasa kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye ananunua kila bao linalofungwa na wawakilishi wa nchi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Kombe la Shirikisho.
Baada ya kukabidhiwa pesa hiyo Bocco amemshukuru Rais Samia na kusema kiasi hicho kimeongeza hamasa kwa wachezaji na kujiona wana deni kila wanaposhuka uwanjani.
“Tunashukuru Mungu kwa kuweza kupata ushindi huu umuhimu ambao umetuweka kwenye nafasi nzuri. Tunamshukuru Rais Samia kwa zawadi hii ambayo inatuongezea morali.
“Pia Tunaishukuru Wizara yetu ya Michezo kwasapoti mnayotupa sisi wachezaji tutapambana kwa ajili ya Simba na nchi kwa ujumla,” amesema Bocco.