Mshambuliaji Chris Mugalu amepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa leo wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs utakaopigwa kwenye Uwanja wa FNB saa moja usiku kwa saa za Tanzania.
Kocha Didier Gomes na wasaidizi wake wamekuwa wakimuamini Mugalu zaidi kuongoza mashambulizi hasa mechi za ugenini kutokana na uwezo wake mkubwa wa kukaa na mpira pamoja na kuwachezesha wenzake.
Kikosi cha leo hakina mabadiliko makubwa kwa jinsi kilivyopangwa hasa kwenye mechi kubwa na muhimu kama ya leo.
Katika eneo la kiungo cha ushambuliaji Gomes amewapanga Clatous Chama, Luis Miquissone na Rally Bwalya huku kwenye ulinzi akiwa na Taddeo Lwanga na Jonas Mkude.
Mlinda mlango Aishi Manula ataendelea kusimama kwenye milingoti mitatu akisaidiwa na walinzi Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Pascal Wawa na Joash Onyango.
Kikosi kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12) Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Pascal Wawa (6), Taddeo Lwanga (4) Clatous Chama (17), Jonas Mkude (20), Chris Mugalu (7), Rally Bwalya (8), Luis Miquissone.
Benchi: Beno Kakolanya (30), David Kameta (27), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Mzamiru Yassin (19), Hassan Dilunga (24), Midie Kagere (14), John Bocco (22), Francis Kahata (25)