Mshambuliaji Chris Mugalu na Clatous Chama wataongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union utakaopigwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga saa 10 jioni.
Wawili hao watapata msaada kutoka kwa viungo washambuliaji wawili Bernard Morrison na Kibu Denis ambao watakuwa wanatokea pembeni.
Taddeo Lwanga ameanza katika kikosi cha kwanza baada ya kupita muda kidogo tangu aliporejea kutoka majeruhi ambapo atakuwa na Sadio Kanoute katika idara ya kiungo wa ulinzi.
Pascal Wawa naye ataanza pamoja na Joash Onyango akichukua nafasi ya Henock Inonga ambaye amepumzishwa.
Kikosi kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Pascal Wawa (6), Taddeo Lwanga (4), Kibu Denis (38), Sadio Kanoute (13), Chris Mugalu (7), Clatous Chama (17), Bernard Morrison (3)
Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Jonas Mkude (20), Mzamiru Yassin (19), Medie Kagere (14), Yusuf Mhilu (27).