Timu ya Mpira Pesa Group kimefanikiwa kuibuka Mabingwa wa Tembo Card Simba Matawi Bonanza baada ya kuichapa Simba Asilia bao moja katika mchezo wa fainali.
Mpira Pesa Group inaundwa na wachezaji wetu wengi wazamani kama Mussa Hassan Mgosi, Emmanuel Gabriel, Juma Jabu, Meshack Abel n wengineo.
Hata hivyo Mpira Pesa Group ilipita kwa njia ya Best Looser kufuatia kupoteza mchezo wa hatua ya pili wa dhidi ya Nguvu ya Simba Asilia.
Mpira Pesa Group ambao ndio Mabingwa wa Tembo Card Simba Matawi Bonanza amejinyakulia pesa taslimu Shilingi milioni mbili, Kombe pamoja na medali.
Kwa upande wao Nguvu ya Simba Asilia yeye atajipatia kitita cha Shilingi milioni moja pamoja na medali.