Mpanzu kuongoza mashambulizi dhidi ya Kagera Sugar

Kiungo mshambuliaji, Elie Mpanzu ataongoza mashambulizi katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa katika Uwanja wa Kaitaba.

Usajili wa Mpanzu umekamilika na tayari hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) imepatikana hivyo yupo huru kuitumikia Simba.

Katika mchezo wa leo kocha Fadlu Davids amefanya mabadiliko ya wachezaji saba ukilinganisha na kile kilichocheza mechi iliyopita dhidi ya Ken Gold.

Fadlu amewaanzisha Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Abdulrazack Hamza, Jean Charles Ahoua, Debora Fernandes, Elie Mpanzu na Steven Mukwala wakichukua nafasi za Kelvin Kijili, Valentine Nouma, Che Malone, Mzamiru Yassin, Ladaki Chasambi, Kibu Denis na Leonel Ateba.

Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:

Moussa Camara (26), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Karaboue Chamou (2), Abdurazack Hamza (14), Fabrice Ngoma (6), Jean Charles Ahoua (10), Debora Fernandes (17), Steven Mukwala (11), Elie Mpanzu (34), Awesu Awesu (23).

Wachezaji wa Akiba

Ally Salim (1), Kelvin Kijili (33), Che Malone (20), Mzamiru Yassin (19), Ladaki Chasambi (36), Yusuph Kagoma (21), Joshua Mutale (7),Leonel Ateba (13), Valentino Mashaka (27), Alexander Erasto (42).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER