Ushindi wa mabao 2-0 tuliopata dhidi ya CS Constantine katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika umetufanya kumaliza vinara wa kundi A.
Tulianza mchezo kwa kasi kwa kuliandama lango la Constantine huku tukitengeneza nafasi kadhaa ambazo hata hivyo hatukuzitumia.
Katika dakika zote 45 za kipindi cha kwanza wageni Constantine walizitumia kujilinda huku wakifika mara mbili langoni kwetu tukimiliki sehemu kubwa ya mchezo.
Kibu Denis alitupatia bao la kwanza dakika ya 60 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kumalizia pasi ya kisigino iliyopigwa na Elie Mpanzu.
Leonel Ateba alitupatia bao la pili dakika ya 80 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi wa kulia Shomari Kapombe.
Ushindi huu umetufanya kufikisha alama 13 tukiwa kileleni mwa msimamo baada ya kucheza mechi sita
X1: Camara, Kapombe, Zimbwe Jr (Nouma 84′) Che Malone, Hamza, Kagoma (Mzamiru 89′), Kibu, Ngoma (Fernandez 84′), Ateba (Balua 89′), Ahoua (Chasambi 84′), Mpanzu
Walioonyeshwa kadi: Kibu 8′ Kagoma 85′
X1: Zakaria, Laid, Benchaira, Baouche, Benchaa (Temine 66′), Dib (Tehar 66′), Meddahi, Merbah, Abraham.(Belhocini 45′), Rebiai, Boudrama
Walioonyeshwa kadi: Baouche 10′ Merbah 34′ Rebiai 61′