Morrison Mchezaji Bora Simba Novemba

Kiungo mshambuliaji, Bernard Morrison amechaguliwa Mchezaji Bora wa Mashabiki wa mwezi Novemba (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

Morrison raia wa Ghana amewashinda mshambuliaji Medie Kagere na kiungo Jonas Mkude ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Katika mwezi Novemba, Morrison amecheza jumla ya dakika ya 235 akifunga mabao mawili na kusaidia kupatikana kwa mengine mawili.

Morrison atakabidhiwa kitita cha Sh 2,000,000 kama sehemu ya zawadi kutoka kwa wadhamini wa tuzo hizo Kampuni ya Emirate Aluminium ACP.

Mchanganuo wa kura ulivyokuwa;

  1. Bernard Morrison kura 2117 (46.77%)
  2. Meddie Kagere kura 2115 (46.73%)
  3. Jonas Mkude kura 294 (6.50%)

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER