Mo Cola yaja na Onja na Ushinde

Klabu ya Simba kwa kushirikiana na Mohamed Interprises Company Limited (Metl) kupitia kinywaji chake cha Mo Cola imekuja na kampeni ya ‘Onja na Ushinde’ ambayo wateja wataweza kujishindia zawadi mbalimbali.

Mkurugenzi wa Masoko kutoka Metl, Fatma Dewji amesema lengo la kampeni hiyo ni kuinua maisha ya Watanzania kwakuwa zawadi ni nyingi na mshindi atakabidhiwa papo hapo.

“Mteja wetu wa Mo Cola akifungua kizibo ndani atakuta zawadi mbalimbali kama soda ya bure, bajaji mpya, pikipiki mpya na pesa taslimu kuanzia 1000 hadi 10,000,000,” amesema Fatma Dewji.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Klabu, Zubeda Hassan amesema Simba kwa kushirikiana na Mo Cola tumedhamiria kuwainua Watanzania kupitia zawadi mbalimbali ambazo watazipata baada ya kununua kinywaji hicho.

“Kampeni ya Onja na na Ushinde itamsaidia kila Mtanzania na sio lazima awe Mwanasimba bali mteja wa Mo Cola kwakuwa ukifungua kizibo utakuweza kupata zawadi mbalimbali,” amesema Bi. Zubeda.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Mo Cola, Imran Haroun amesema zawadi kama soda na pesa kuanza 1000 hadi 10,000 mteja atapewa papo hapo lakini zile kubwa kama bajaji, pikipiki na milioni 10 zitakabidhiwa ofisi za Metl.

“Kuna aina mbili za zawadi kubwa na ndogo zile kubwa zitatolewa ofisini kwa utaratibu utakaopangwa lakini zile ndogo mteja atakabidhiwa pale pale baada ya kufungua kizibo,” amesema Bw. Imaran.

Uzinduzi wa kampeni hiyo ambayo itadumu kwa miezi mitatu kuanzia Januari mpaka Machi 2025 ilihudhuriwa na wachezaji Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ Fabrice Ngoma, Shomari Kapombe na Awesu Awesu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER