Rais wa Klabu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohamed Dewji ‘Mo’ amekutana na kocha Fadlu Davids kwa ajili ya kujadiliana kuhusu msimu ulivyokuwa na mipango thabiti kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025/2026.
Mo amemuhakikishia Fadlu kuwa atahakikisha kila mchezaji atakaye mpendekeza atamsajili ili kuwa na kikosi imara huku akiahidi Simba ya msimu ujao haitazuilika.
“Nimefurahi kuwa na mazungumzo na Kocha Fadlu katika msimu wake wa kwanza, akiwa na kikosi kipya na benchi jipya la ufundi, ameiongoza Simba SC kufika fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF.”
“Chini ya Kocha Fadlu Simba imefika fainali ya CAF Confederation Cup, fainali ya pili ya kimataifa katika historia ya klabu. Msimu huu ulikuwa wa kujenga timu na bado tukafika fainali, licha ya upinzani mkali na matumaini yetu ni kufanya vizuri zaidi msimu huu,” amesema Mo.