Kiungo mshambuliaji, Yusufu Mhilu, amejiunga na kikosi chetu kutoka Kagera Sugar kwa mkataba wa miaka mitatu.
Mhilu amekuwa kwenye kiwango bora tangu alipojiunga na Kagera na kulivutia benchi letu la ufundi chini ya Kocha Didier Gomes lililopendekeza usajili wake.
Mhilu anakuwa mchezaji wa pili kujiunga nasi msimu huu baada ya kiungo Peter Banda ambaye tulimtambulisha jana kutoka Big Bullet ya Malawi.
Msimu huu tumepanga kufanya usajili wa kisayansi wa kuongeza wachezaji katika nafasi muhimu lengo ni kuhakikisha tunatwaa tena ubingwa wa michuano yote yaani Ligi Kuu, Azam Sports Federation Cup na kufanya vizuri Ligi ya Mabingwa Afrika.
One Response
No comment