Mgeni Rasmi, Waziri wa Maji, Mh. Jumaa Aweso ameusifu Uongozi wa klabu kwa kuandaa Tamasha bora la Simba Day ambalo haijawahi kutokea kabla.
Mh. Aweso amesema ameshiriki Simba Day nyingi huko nyuma lakini hii ya mwaka 2025 ni bora na tofauti kuliko za nyuma kuanzia mpangilio mpaka burudani.
Mh. Awesu ameongeza kuwa alipopata barua ya mwaliko yakuwa mgeni rasmi wa Simba Day hakusita kwakuwa siku hii inamuhusu moja kwa moja sababu yeye ni Mwanasimba kindaki ndaki.
“Hii haijawahi kutokea, nimewahi kushiriki Simba Day kadhaa huko nyuma lakini hii ni tofauti. Waswahili wanasema iga ufe, hata mdogo wangu Ahmed Ally ulivyoingia uwanjani ni kivingine haijawahi kutokea,” amesema Mh. Aweso.
Mh. Aweso amewasisitiza Viongozi, Benchi la Ufundi na wachezaji kuwa kwa sasa kinachohitajika ni kutwaa mataji sababu timu ni nzuri na Wanasimba wanataka furaha na wanastahili.