Mgunda: Ya Tabora yameisha tunajiandaa na Azam

Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mgunda amesema baada ya ushindi wa mabao 2-0 tuliopata dhidi ya Tabora United sasa tunajipanga kwa ajili ya mechi inayofuata na Azam FC.

Mgunda amesema mchezo dhidi ya Tabora ulikuwa mgumu na walitupa upinzani mkubwa lakini umemalizika na tunajipanga kwa mechi ya Azam.

“Kila mchezo una maandalizi yake, huu wa leo umeisha tunarudi mazoezini kujiandaa na mechi inayofuata,” amesema Mgunda.

Akizungumzia mchezo wenyewe Mgunda amesema “hii ni mechi muhimu kwakuwa itaamua nani anatakiwa kukaa juu ya mwenzie.”

“Kitu kingine msisahau kuwa hii ni Derby ambayo inatakutanisha timu bora ambazo zinapigania ubingwa, kwahiyo haiwezi kuwa rahisi lakini tumejipanga kwa ajili ya mchezo huo,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER