Kocha Mkuu Juma Mgunda amesema maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa kesho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 12:15 jioni yamekamilika.
Mgunda amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na ukiwatoa wale ambao ni majeruhi wa muda mrefu lakini wengine wote wapo tayari kwa mchezo.
Amesema mchezo utakuwa mgumu Prisons ni timu nzuri na tutaingia uwanjani tukiwa tunajua tutapata upinzani mkubwa lakini tumejiandaa kikamilifu kuhakikisha tunapata pointi zote tatu.
“Maandalizi yote ya mchezo yamekamilika wachezaji wapo kwenye hali nzuri, tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tupo tayari kupambana,” amesema Mgunda.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji, mlinzi wa kushoto Gadiel Michael amesema kila kitu sawa kwa upande wao na yeyote atayepata nafasi atakuwa tayari kuitumikia timu.
“Sisi wachezaji tupo tayari kwa mchezo, morali zipo juu. Tunawaheshimu Prisons ni timu nzuri lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata pointi zote,” amesema Gadiel.
One Response
Kila laeli kwenu timu yangu mwenyezi mungu awafanyie wepesi kwenye mechi hii