Kocha Msaidizi wa Simba Queens, Mussa Hassan Mgosi amesema kikosi chetu kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Wanawake dhidi ya Geita Queens utakaopigwa katika Uwanja wa Nyankumbu saa 10 jioni.
Mgosi amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo na malengo yakiwa kuchukua pointi tatu katika kila mechi.
Mgosi ameongeza malengo ya mwaka 2024 ni kurejesha heshima ya Simba Queens ambayo tuliipoteza mwaka jana.
“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Geita, tunafahamu utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda,” amesema Magosi.
Akizungumzia kupata pointi tatu baada ya JKT Queens kutotokea uwanjani Mgosi amesema “mpira wa miguu unachezwa kwa kanuni sisi tulijua tutapata pointi zile lakini hata kama isingekuwa hivi kama wangekuja uwanjani bado tungeshinda,” amesema Mgosi.