Mechi dhidi ya USGN kupigwa saa nne usiku

Mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gandarmerie utapigwa saa nne usiku badala ya saa moja kama ilivyokuwa imetangazwa.

Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika saa moja usiku lakini kwa mujibu wa taarifa tuliyopata kutoka Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) mechi itapigwa saa nne usiku.

Tayari kikosi kipo kambini kuendelea na maandalizi ya mchezo huo muhimu ambapo kwetu tunauchukulia kama fainali sababu lengo letu ni kutinga robo fainali ya michuano hii.

Viingilio vya mchezo huu vimepangwa kama ifuatavyo

Mzunguko Sh 3,000

VIP C Sh 10,000

VIP B Sh 20,000

VIP A Sh 30,000

Platinum Sh 150,000

Uongozi unaendelea kusisitiza mashabiki kununua tiketi mapema kupitia kwenye mitandao ya simu ili kuepusha usumbufu siku ya mchezo.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER