Mechi dhidi ya Azam kupigwa Benjamin Mkapa

Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) imebadili uwanja na muda mchezo wetu namba 167 wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC ambao ulipangwa kufanyika Jumatatu saa 10 jioni katika Uwanja wa KMC Complex sasa utapigwa katika dimba la Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Taarifa ya TPLB imesema sababu ya kuutoa mchezo huo kutoka katika Uwanja wa KMC Complex kuupeleka Benjamin Mkapa ni kutokana na ukubwa wa mechi ambao tunategemea mashabiki watakuwa wengi.

Msimu huu tumechagua Uwanja wa KMC Complex kwa ajili ya mechi zetu za nyumbani lakini kutokana na ukubwa wa mchezo TPLB imeupeleka katika dimba la Benjamin Mkapa ambalo lina uwezo wa kuingiza mashabiki 60,000.

Maandalizi ya mchezo huo ambao tunaamini utakuwa mgumu kutokana na ubora wa Azam yanaendelea vizuri na malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda na kuchukua alama tatu.

Viingilio vya mchezo ni kama ifuatavyo:

VIP A Sh. 30,000
VIP B Sh. 20,000
Machungwa Sh.10,000
Mzunguko Sh. 5,000

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER