Mchezo dhidi ya JKT kupigwa Disemba 24

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeupangia tarehe mchezo wetu namba 79 dhidi ya Maafande wa JKT Tanzania ambao sasa utapigwa Disemba 14 katika Uwanja wa KMC Complex saa 10 jioni.

Awali mchezo huo ulikuwa umepangwa kuchezwa katika Uwanja wa KMC Complex, Oktoba 29 lakini basi lililokuwa limebeba wachezaji wa JKT lilipata ajali wakati wakirejea kutoka Dodoma hali iliyofanya mchezo kuahirishwa.

Baada ya taarifa hiyo rasmi kutoka Bodi ya Ligi ni kwamba baada ya mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar ugenini Disemba, 21 tutarejea Dar es Salaam kucheza na JKT.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER