Mchezo dhidi ya Azam kupigwa Septemba 26

Mechi ya Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC ambao ulikuwa haukupangiwa tarehe sasa utapigwa Septemba 26.

Baada ya ratiba hiyo sasa ni rasmi mchezo huo ambao unamsubiriwa kwa hamu utapigwa Alhamisi ya Septemba 26 saa 12 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Bodi ya Ligi leo imeweka wazi tarehe ya michezo mbalimbali ambayo ilikuwa haijapangiwa kutokana na sababu tofauti.

Mchezo huo ulichelewa kupangiwa tarehe kutokana na ushiriki wa michuano ya Afrika kwa timu zote.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER