Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya watani wajadi Yanga.
Mapema mchana wa leo wakati akizungumza na Wanahabari kuelekea mchezo huo kocha Mkuu Fadlu Davids amesema pamoja na ukubwa na presha ya mechi lakini tutacheza kwa mipango yetu.
Kocha Fadlu amesema ingawa wachezaji wengi ni wageni na hawakucheza mechi nyingi za ‘Dabi’ lakini wapo tayari kutoa kila kitu kwa ajili ya kuisaidia timu kupata ushindi.
“Kikosi kipo kwenye hali nzuri na wachezaji wote wameshiriki mazoezi ya mwisho na kesho tutakuwa na wigo mpana wa kuchagua nani aanze,” amesema Kocha Fadlu.