Mazembe mshindi Simba Day

Kikosi chetu kimepoteza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya TP Mazembe katika kilele cha Tamasha la Simba Day lililofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ulianza taratibu huku timu zote zikisomana na kufanya mashambulizi ya kushtukiza huku mpira ukichezwa zaidi katikati ya uwanja.

Dakika ya 29 almanusura Chris Mugalu atupatie bao la kuongoza baada ya shambulizi safi lilofanywa na Bernard Morrison na Rally Bwalya lakini shuti lake lilipaa juu ya lango.

Mazembe walipata bao dakika ya 84 kupitia kwa Baleke Jean kufuatia mlinda mlango Aishi Manula kutoka katika eneo lake.

Baada ya bao hilo tuliongeza mashambulizi langoni mwa Mazembe lakini safu yao ya ulinzi ilikuwa imara kuhakikisha inaondoa hatari zote.

Kocha Didier Gomes aliwatoa Morrison, Kibu Denis Mugalu, Taddeo Lwanga, Bwalya, Saido Kanoute, Shomari Kapombe na Mohammed Hussein.

Nafasi zikachukuliwa na Pape Ousmane Sakho na Peter Banda, John Bocco, Erasto Nyoni, Medie Kagere, Henock Inonga na Duncan Nyoni.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

  1. Pingback: My Homepage

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER