Kocha Msaidizi Seleman Matola amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa fainali dhidi ya wenyeji Al Hilal utakaopigwa kesho katika Uwanja wa Al Hilal nchini Sudan saa mbili usiku.
Matola amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na kikosi kimeongezewa nguvu baada ya kuwasili kwa Nahodha John Bocco na kiungo Sadio Kanoute.
Matola ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu kutokana na wenyeji Al Hilal kutaka kulipa kisasi kwetu baada ya kuwafunga mara kadhaa tulipokutana katika miaka ya karibuni.
“Kikosi kipo kamili, wachezaji wapo kwenye hali nzuri jana tumefanya mazoezi na leo na tunashukuru hakuna aliyepata majeraha ambayo yatamfanya kukosa mchezo wa kesho.
“Nahodha Bocco na Kanoute wamejiunga na kikosi na tunategemea watakuwa sehemu ya mchezo wetu wa kesho. Tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Matola.