Matola: Tumejiandaa kucheza vizuri mechi za mwisho

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema wachezaji wetu wameandaliwa kimwili na kiakili kucheza mechi hizi za mwisho wakati ligi ikiwa inaelekea ukingoni.

Matola amesema ligi inapokuwa inaelekea mwisho ugumu unaongezeka kwakuwa kila timu inataka kushinda ili kujiweka kwenye nafasi nzuri lakini tupo tayari kupambana na kila kilichopo mbele yetu ili kufikia malengo.

Akizungumzia mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya JKT Tanzania, Matola amesema utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani ila malengo yetu ni kupata pointi tatu.

“Haitakuwa mechi rahisi, tunakutana na timu yenye wachezaji wengi wazoefu na wanaijua vizuri ligi lakini Simba ni timu kubwa na tupo tayari kupambana na kila changamoto iliyo mbele yetu,” amesema Matola.

Nae mlinzi wa kulia David Kameta ‘Duchu’ amesema pamoja na ugumu ambao tunaenda kukutana nao lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

“Kila mchezo kwetu ni fainali, Simba ina wachezaji wazuri na wenye uzoefu mkubwa na mechi kama hizi. Tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda na kuchukua pointi zote tatu ugenini,” amesema Duchu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER