Matola: Tulistahili kushinda

Kaimu Kocha Mkuu Seleman Matola, amesema ushindi tuliopata dhidi KMC tulistahili kutokana na kiwango kikubwa kilichoonyeshwa na wachezaji wetu.

Matola amesema tulicheza vizuri muda wote na wachezaji walijitahidi kufuata maelekezo aliyowapa.

Matola ameongeza kuwa kipindi cha kwanza KMC waliingia kwa njia ya kuzuia hivyo wote wakawa nyuma ya mpira lakini kipindi cha pili walivyofunguka tukaweza kuwafunga.

“Ukiangalia mchezo mzima sisi tulikuwa bora zaidi yao, tulitengeneza nafasi nyingi na tulistahili kupata ushindi kwa kuwa tulicheza vizuri.

“KMC walitusumbua kipindi cha kwanza kwa kuwa wote walikuwa nyuma walikuwa wanazuia tu lakini tulivyorudi cha pili tulitafuta njia za kuwafungua na kufanikiwa kupata mabao yote matatu,” amesema Matola.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER