Kocha, Selemani Matola leo ameanza mazoezi kazi na ameshiriki katika mazoezi ya jioni wakati kikosi kikijiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo.
Matola amerejeshwa kikosini baada ya klabu kuachana na kocha mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ jana ambapo sasa atasaidiana na Daniel Cadena.
Wakati Robertinho anajiunga nasi Januari mwaka huu, Matola alienda masomoni na alipomaliza alipewa majukumu ya timu ya vijana kabla ya jana kupandishwa timu ya wakubwa.
Matola ambaye alikuwa nahodha wa timu yetu mara kadhaa amekiongoza kikosi chetu.