Mamia ya mashabiki wamejitokeza kwa wingi kushiriki mbio za Hisani (Fun Run) zenye urefu wa kilomita sita kutoka Coco Beach hadi Sea Clieff na kurudi tena Coco Beach.
Mbio hizo za Hisani ni moja ya matukio tuliyokuwa tumeyapanga kuyafanya katika wiki hii ya Simba kuelekea kilele cha Simba Day siku ya Jumatano, Septemba 10.
Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amewapongeza waliojitokeza kushiriki mbio hizo huku akiahidi tutaendelea kuzifanya mara kwa mara kwakuwa inaonekana wengi wamependa.
Ahmed amesema kuelekea kwenye mechi zetu za Kimataifa msimu huu tutafanya matukio mbalimbali kama haya ili kuzidi kuwafanya Wanasimba kuwa kitu kimoja na kuongeza mshikamano.
“Kipekee niwashukuru wote mliojiyokeza kushiriki mbio hizi, najua mmeacha shughuli zenu kuna wengine mmeacha kwenda kwenye ibada kwa ajili ya jambo hili kiukweli mmetutia moyo.
“Hii ni mara ya kwanza kwetu kufanya jambo hili, tutaenda kukaa chini na kuangalia mapungufu yaliyojitokeza ili tukifanya wakati mwingine iwe kubwa zaidi,” amesema Ahmed.