Magori: Hatujafanyiwa figisu nchini Botswana

Mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu, Crescentius Magori amesema hatujafanyiwa hujuma yoyote katika mchezo wetu wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy nchini Botswana uliopigwa Jumapili iliyopita.

Magori amesema kila kitu kilikwenda sawa na wenyeji wetu hawakufanya jambo lolote nje uwanja ambalo unaweza kulitafsiri kama hujuma au figisu.

Magori ambaye amerejea nchini leo alfajiri kutoka Botswana ameweka wazi kuwa kwa sasa nguvu yetu tunaelekeza kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Licha ya kufanikiwa kuondoka na mtaji wa mabao mawili ugenini Magori amesisitiza mechi bado haijaisha na Jwaneng si timu mbaya kama wengi wanavyodhani hivyo tunapaswa kuingia kwa makini ili kupata tiketi ya kuingia hatua ya makundi.

“Kila kitu kilienda sawa kule Botswana, hakukuwa na hujuma yoyote wala figisu na vita ilikuwa uwanjani pekee. Kwa sasa macho yetu na nguvu ni kuelekea mechi ya marudiano wiki ijayo,” amesema Magori.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER