Leo tupo Lake Tanganyika kuikabili Mashujaa FC

Kikosi chetu leo saa 10 jioni kitashuka katika Uwanja wa Lake Tanganyika kuikabili Mashujaa FC katika muendelezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Tutaingia katika mchezo wa leo tukiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 3-0 tuliopata dhidi ya Namungo FC katika mechi iliyopita.

Tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Mashujaa hasa tukiwa tunafahamu wapo nyumbani lakini tupo tayari kuwakabili ili kupata pointi zote tatu.

Matola aweka mambo wazi…..

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema mara zote mchezo dhidi ya Mashujaa haujawahi kuwa mwepesi kwetu na tunakumbukumbu ya kutolewa kwenye michuano ya CRDB Bank Federation Cup tulivyokutana mara ya mwisho msimu uliopita.

Matola ameongeza pamoja nakuwa na wachezaji wengi hawakuwepo katika mchezo uliopita lakini wanafahamu ugumu na umuhimu wa kupata pointi tatu kwenye mechi ya leo.

“Ni mechi ngumu. Mashujaa ni timu bora hasa inapokuwa katika uwanja wa nyumbani lakini tumechukua tahadhari zote huku lengo likiwa kuondoka na pointi tatu,” amesema Matola.

Mzamiru afunguka……

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mkabaji, Mzamiru Yassin amesema licha ya kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo uliopita lakini sisi bado ni bora zaidi yao.

Mzamiru amesema daraja ilipo Simba ni juu zaidi ya Mashujaa ingawa kwenye mpira ubora wa dakika 90 ndio unaamua mechi.

“Itakuwa mechi ngumu lakini Simba ni bora zaidi ya Mashujaa na sisi hatupiganii nafasi ya pili au ya tatu bali ubingwa kwahiyo kila mechi kwetu ni fainali,” amesema Mzamiru.

Nyota wanne kuikosa Mashujaa

Mlinda mlango Aishi Manula hayupo kwenye kikosi cha leo kutokana nakuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa inayojiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za CHAN dhidi ya Sudan.

Wengine ni mlinda mlango Ayoub Lakred, mlinzi Abdulrazack Hamza na kiungo mkabaji Yusuph Kagoma ambao ni majeruhi.

Tulipata ushindi Lake Tanganyika mara mwisho….

Mara ya mwisho kucheza mechi ya Ligi dhidi ya Mashujaa katika Uwanja wa Lake Tanganyika ilikuwa Februari 3, mwaka huu na tuliibuka na ushindi wa bao moja lililofungwa na Said Ntibazonkiza kwa mkwaju wa penati.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER