Lakred ni Mnyama

Mlinda mlango, Ayoub Lakred (28) raia wa Morocco amejiunga na kikosi chetu kutoka FAR Rabat kwa mkataba wa miaka miwili.

Lakred ambaye ni mlinda mlango kiongozi amewahi pia kuitumikia RS Berkane ya nchini Morocco.

Lakred ana uzoefu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo tunaamini atakuwa msaada mkubwa.

Lakred ameiongoza FAR Rabat kushinda ubingwa wa Morocco msimu uliopita na kuifikisha Nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Lakred anakuja kuungana na Ally Salim, Hussein Abeli na Ahmed Feruz kipindi hiki mlinda mlango Aishi Manula akiendelea kuuguza jeraha lake.

Tunategemea uwezo wa Lakred utaimarisha lango letu kuelekea kuanza msimu mpya wa mashindano.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER