Uongozi wa klabu unatangaza kufikia makubaliano ya kuachana na kiungo mkabaji Victor Akpan raia wa Nigeria.
Akpan alijiunga nasi Julai, 2022 akitokea Coastal Union lakini baada ya uboreshaji mkubwa wa kikosi ambao tumepanga kuufanya kwenye kikosi chetu msimu huu benchi la ufundi limeona hatakuwa sehemu ya mipango yake.
Novemba mwaka jana tulimtoa kwa mkopo katika klabu ya Ihefu FC lakini sasa tumefikia makubaliano ya kuachana moja kwa moja
Simba inamshukuru Akpan kwa utumishi wake ndani ya timu pia inamtakia kheri kwenye maisha yake mapya ya soka nje ya kikosi chetu.
Tunaendelea kuboresha timu kuelekea msimu mpya wa Ligi 2023/24 na lengo letu nikuwa na timu imara yenye ushindani itakayokuwa na uwezo wa kuchukua ubingwa.