Kwaheri Valentin Nouma

Baada ya makubaliano ya pande mbili tumevunja mkataba na mlinzi wa kushoto Valentin Nouma raia wa Burkina Faso.

Nouma tumemsajili kutoka St. Eloi Lupopo ya DR Congo msimu uliopita kwa mkataba wa miaka mitatu lakini sasa baada ya makubaliano haya hatakuwa sehemu ya kikosi chetu katika msimu wa mashindano 2025/2026.

Katika kipindi cha mwaka mmoja ambacho Nouma alikuwepo kikosini amekuwa mchezaji muhimu akisaidiana na nahodha, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.

Miongoni mwa sifa alizokuwanazo Nouma ni uwezo wake wa kuzuia pamoja na kushambulia huku pia akiwa na uzoefu mkubwa wa kufunga kwa mipira ya adhabu.

Uongozi wa klabu unamtakia Kheri Nouma katika maisha yake mapya ya soka nje ya Simba.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER