Kwaheri Che Fondoh Malone

Mlinzi wa kati, Che Fondoh Malone hatakuwa sehemu ya kikosi chetu kuelekea msimu mpya wa mashindano 2025/2026 baada ya kujiunga na USM Algiers ya Algeria kwa mkataba wa kudumu.

Che Malone alijiunga nasi Julai 2023 kutoka Cotton Sports ya Cameroon na tangu hapo amekuwa muhimili mkubwa katika idara yetu ya ulinzi.

Che Malone (26) raia wa Cameroon alikuwa amebakisha mkataba wa mmoja lakini baada ya makubaliano baina yetu pamoja na USM Algiers sasa ni rasmi amejiunga na miamba hiyo ya Algeria.

Klabu ya Simba imekuwa muumini mkubwa wa kuwapa wachezaji wake nafasi kila kunapo patikana fursa mpya ili kuwafanya kupata mafanikio zaidi ya kiuchumi.

Simba inamtakia kheri Che Malone katika maisha yake mapya ya soka katika timu ya USM Algiers.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER