Baada ya makubaliano ya pande mbili kiungo mkabaji raia wa Nigeria, Augustine Okejepha hatakuwa sehemu ya kikosi chetu kuelekea msimu ujao wa Ligi 2025/2026.
Okejepha 25, amejiunga nasi msimu uliopita akitokea Rivers United ya nchini kwao Nigeria kwa mkataba wa miaka miwili ambao umefikia tamati baada ya makubaliano.
Okejepha ni mchezaji mwenye uwezo na kipaji kikubwa ingawa hakuweza kupata muda mwingi wa kucheza.
Simba inamtakia kheri na mafanikio mema katika maisha yake mapya nje ya kikosi chetu.