Kocha Matola afunguka kuelekea mchezo dhidi ya Mashujaa

Kocha Msaidizi, Seleman Matola ameweka wazi kuwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mashujaa FC utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda.

Matola amesema kwa sasa kila mchezo tunauchukulia kwa umakini mkubwa na tunahitaji kupata pointi tatu ili kufikia malengo yetu ya kutwaa ubingwa.

Akizungumzia ugumu wa ratiba, Matola amesema tutafanya mabadiliko ya wachezaji mara kwa mara ili kuwapumzisha kwakuwa tuna mechi nyingi ambazo zipo karibu karibu.

“Tunategemea mchezo mgumu kutoka kwa Mashujaa lakini tumejiandaa na tupo tayari kupambana mpaka mwisho ili kupata pointi tatu.”

“Tunafahamu tuna ratiba ngumu lakini tuna kikosi imara ambacho tunaweza kuwagawa wachezaji kulingana na mechi na bado tukapata matokeo chanya,” amesema Matola.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mshambuliaji, Awesu Awesu amesema kila mchezo kwetu ni fainali na malengo yetu ni kupata pointi tatu.

“Tangu tumeanza msimu huu mechi zote tulizocheza ni ngumu na hata ya kesho itakuwa ngumu lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda,” amesema Awesu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER