Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja Sokoine kuikabili Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefanya mabadiliko ya wachezaji wawili ukilinganisha na kikosi kilichocheza mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Power Dynamos.
Mlinda mlango Ally Salim ameanza mbele ya Ayoub Lakred na nahodha John Bocco amechukua nafasi ya Jean Baleke.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Ally Salim (1), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Kennedy Juma (26), Che Malone (20), Mzamiru Yassin (19), Fabrice Ngoma (6), Clatous Chama (17), John Bocco (22), Said Ntibazonkiza (10), Kibu Denis (38).
Wachezaji wa Akiba
Ayoub Lakred (36), Israel (5), Hussein Kazi (16), Sadio Kanoute (8), Abdallah Hamisi (13), Willy Onana (7), Shaban Chilunda (27), Jean Baleke (4), Moses Phiri (25).