Leo saa 9:30 jioni tutashuka dimbani kuikabili Singida Black Stars katika mchezo wa nusu fainali ya CRDB Federation Cup katika mtanange utakaopigwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa.
Kocha Fadlu, Davids amefanya mabadiliko ya wachezaji wanne ukilinganisha na kikosi kilichoanza mechi iliyopita dhidi ya Singida.
Fadlu amewaanzisha David Kameta ‘Duchu’, Valentine Nouma, Abdulrazack Hamza na Kibu Denis kuchukua nafasi za Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Karaboue Chamou na Elie Mpanzu.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Moussa Camara (26), David Kameta (3), Valentin Nouma (29), Che Malone Fondoh (20), Abdurazak Hamza (14), Yusuph Kagoma (21), Kibu Denis (38), Fabrice Ngoma (6), Steven Mukwala (11), Jean Charles Ahoua (10), Joshua Mutale (7).
Wachezaji wa Akiba:
Ally Salim (1), Mohamed Hussein (15), Karaboue Chamou (2), Augustine Okajepha (25), Ladaki Chasambi (36), Deborah Fernandes (17), Awesu Awesu (23), Valentino Mashaka (27), Bashir Salum (59). Elie Mpanzu (34).