Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya RS Berkane Leo

Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Amaan Zanzibar kuikabili RS Berkane katika mchezo wa mkondo wa pili wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kocha Mkuu Fadlu Davids amefanya mabadiliko ya mchezaji watatu ukilinganisha na kikosi kilichoanza mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa nchini Morocco wiki iliyopita.

Fadlu amewaanzisha Che Fondoh Malone, Joshua Mutale na Steven Mukwala kuchukua nafasi za Abdulrazack Hamza, Kibu Denis na Leonel Ateba.

Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:

Moussa Camara (40), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Karaboue Chamou (2), Che Malone (20), Yusuph Kagoma (21), Joshua Mutale (26), Fabrice Ngoma (6), Steven Mukwala (11), Jean Charles Ahoua (10), Elie Mpanzu (34).

Wachezaji wa Akiba:

Ally Salim (1), David Kameta (3), Valentine Nouma (29), Augustine Okajepha (25), Ladaki Chasambi (36), Deborah Fernandes (17), Leonel Ateba (13), Awesu Awesu (23), Kibu Denis (38).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER