Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Prisons leo

Mabeki Mohamed Hussein na Joash Onyango wamerejea katika kikosi kilichopangwa kuikabili Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa Uwanja kwa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Walinzi hao pamoja na mlinda mlango Aishi Manula hawakucheza mechi iliyopita ya hatua ya 32 bora ya Michuano ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Dar City ambayo tuliibuka na ushindi wa mabao 6-0.

Katika eneo la kiungo Mzamiru Yassin ambaye pia hakuanza kwenye mchezo uliopita naye ameingia kikosini ambapo atasaidiana na Erasto Nyoni kukaba.

Kikosi kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Erasto Nyoni (18), Hassan Dilunga (24), Mzamiru Yassin (19), Medie Kagere (14), Clatous Chama (17), Rally Bwalya (8)

Kikosi cha Akiba

Beno Kakolanya (30), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Pascal Wawa (6), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (10), John Bocco (22), Chris Mugalu (7), Jimmyson Mwinuke (21)

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER