Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Mbeya City

Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa KMC Complex kuikabili Mbeya City katika mchezo wa robo fainali ya CRDB Federation Cup.

Kocha Mkuu, Fadlu Davids amefanya mabadiliko ya wachezaji nane ukilinganisha na kile kilichocheza wikiendi iliyopita mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry.

Ni nyota watatu tu ambao walianza dhidi ya Al Masry ambao ni Karaboue Chamou, Abdulrazack Hamza na Fabrice Ngoma na wameanza tena leo mbele ya Mbeya City.

Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa

Ally Salim (1), David Kameta (3), Valentin Nouma (29), Karaboue Chamou (2), Abdurazak Hamza (14), Fabrice Ngoma (6), Ladaki Chasambi (36), Debora Fernandes (17), Leonel Ateba (13), Awesu Awesu (13), Joshua Mutale (7),

Wachezaji wa Akiba:

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (2), Yusufu Kagoma (21), Augustine Okejepha (25), Edwin Balua (37), Elie Mpanzu (34), Steven Mukwala (11), Denis Kibu (38), Alexander Erasto (42), Adolf Hamisi (50).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER