Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Mbeya City

Mshambuliaji Kibu Denis ataongoza safu ya ushambuliaji katika mchezo wa wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Kibu apata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Rally Bwalya na Pape Ousmane Sakho.

Erasto Nyoni amepangwa kama kiungo mkabaji pamoja na Mzamiru Yassin na Sadio Kanoute.

Henock Inonga na Pascal Wawa watasimama kama mabeki wakati huku nahodha Mohamed Hussein na Israel Patrick wakicheza pembeni.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (15), Henock Inonga (29), Pascal Wawa (6), Erasto Nyoni (18), Mzamiru Yassin (19), Sadio Kanoute (13), Kibu Denis (38), Rally Bwalya (8), Pape Sakho (10)

Wachezaji wa Akiba

Ally Salim (1), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Taddeo Lwanga (4), Yusuf Mhilu (27), Medie Kagere (14), Peter Banda (11), Jimmyson Mwanuke (21).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER