Kibu Denis amepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa pili wa kirafiki dhidi ya Kipanga FC utakaopigwa Uwanja wa Amaan Zanzibar saa 2:15 usiku.
Kibu atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Jimmyson Mwanuke, Nelson Okwa na Augustine Okrah.
Jonas Mkude na Nassor Kapama wataendelea kuongoza safu ya kiungo huku Joash Onyango na Erasto Nyoni wakisimama kama walinzi wa kati.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Ally Salim (1), Israel Patrick (5), Gadiel Michael (2), Joash Onyango (16), Erasto Nyoni (18), Jonas Mkude (20), Jimmyson Mwanuke (21), Nassor Kapama (35), Kibu Denis (38), Nelson Okwa (8), Augustine Okrah.
Wachezaji wa Akiba
Ahmed Feruzi (31), Mohamed Hussein (15), Kennedy Juma (26), Victor Akpan (6), John Bocco (22), Moses Phiri (25).