Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Kagera Leo

Kikosi chetu leo saa 10 jioni kitashuka katika Uwanja wa Uhuru kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha amefanya mabadiliko ya wachezaji watatu ukilinganisha na kile kilichoanza mchezo wa mwisho tuliocheza dhidi ya Wydad Casablanca.

Benchikha amewaanzisha Mzamiru Yassin, Moses Phiri na Clatous Chama wakichukua nafasi za Kibu Denis, Jean Baleke na Willy Onana.

Kikosi kamili kilivyopangwa:

Ayoub Lakred (40), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Che Malone (20), Henock Inonga (29), Fabrice Ngoma (6), Mzamiru Yassin (19), Sadio Kanoute (8), Moses Phiri (25), Said Ntibazonkiza (10), Clatous Chama (17).

Wachezaji wa Akiba:

Ally Salim (1), Israel Patrick (5), Kenedy Juma (26), Jimmyson Mwanuke (21), Kibu Denis (38), Willy Onana (7), Jean Baleke (4), John Bocco (22).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER