Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kuikabili JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC
Kocha Fadlu Davids amefanya mabadiliko ya wachezaji sita ukilinganisha na kikosi kilichocheza mechi iliyopita dhidi ya Mashujaa.
Fadlu amewaanzisha Shomari Kapombe, Fabrice Ngoma, Kibu Denis, Steven Mukwala, Jean Charles Ahoua na Joshua Mutale wakichukua nafasi za David Kameta, Yusuph Kagoma, Edwin Balua, Leonel Ateba, Awesu Awesu na Elie Mpanzu.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Moussa Camara (26), Shomari Kapombe (12), Valentin Nouma (29), Karaboue Chamou (2), Abdurazak Hamza (14), Fabrice Ngoma (6), Kibu Denis (38), Debora Fernandes (17), Steve Mukwala (11), Jean Charles Ahoua (10), Joshua Mutale (7).
Wachezaji wa Akiba:
Ally Salim (1), Mohamed Hussein (15), Che Malone Fondoh (20), Augustine Okejepha (25), Yusuph Kagoma (21), Leonel Ateba (13), Ladack Chasambi (36), Alexander Erasto (42), Adolf Hamis (50), Elie Mpanzu (34).