Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Gaborone United

Leo saa mbili usiku kikosi chetu kitashuka katika uwanja Obedi Itani Chilume nchini Botswana kuikabili Gaborone United katika mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha Mkuu Fadlu Davids amefanya mabadiliko ya wachezaji wanne ukilinganisha na kile kilichoanza mechi ya Ngao ya Jamii wikiendi iliyopita.

Fadlu amewaanzisha Anthony Mligo, Karaboue Chamou, Seleman Mwalimu na Neo Maema na wakichukua nafasi za Abdulrazak Hamza, Yusuph Kagoma, Kibu Denis na Steven Mukwala.

Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:

Moussa Camara (26), Shomari Kapombe (12), Anthony Mligo (5), Karaboue Chamou (2), Rushine De Reuck (23), Allasane Kante (8), Elie Mpanzu (34), Naby Camara (30), Seleman Mwalimu (40), Jean Charles Ahoua (10), Neo Maema (35).

Wachezaji wa Akiba:

Yakoub Suleiman (22), Ladaki Chasambi (36), Wilson Nangu (31), Mzamiru Yassin (19), Kibu Denis (38), Morice Abraham (18), Steven Mukwala (11), Jonathan Sowah (3), Joshua Mutale (7).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER