Nahodha John Bocco, ataendelea kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa mwisho wa kirafiki hapa Mjini Dubai dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi utakaopigwa Abu Dhabi saa tisa Alasiri.
Kama ilivyokuwa katika mchezo uliopita dhidi ya Al Dhafrah, Bocco atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Clatous Chama, Saido Ntibazonkiza na Pape Sakho.
Katika eneo la kiungo wa ulinzi kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amempanga Erasto Nyoni pamoja na Sadio Kanoute.
Kikosi kamili kilivyopangwa
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Mohamed Ouattara (33), Erasto Nyoni (18), Pape Sakho (10), Sadio Kanoute (13), John Bocco (22), Saido Ntibazonkiza (39), Clatous Chama (17).
Wachezaji wa Akiba
Beno Kakolanya (30), Ally Salim (1), Jimmyson Mwanuke (21), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Nassor Kapama (35), Jonas Mkude (20), Mzamiru Yassin (19), Habibu Kyombo (32), Kibu Denis (38)