Leo saa 10 jioni tutashuka katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuikabili Coastal Union katika mchezo wa 21 wa Ligi Kuu ya NBC.
Kocha Mkuu, Fadlu Davids amefanya mabadiliko ya wachezaji sita ukilinganisha na kikosi kilichoanza mechi iliyopita dhidi ya Azam FC.
Kocha Fadlu amewaanzisha Ally Salim, David Kameta ‘Duchu’, Valentine Nouma, Chamou Karaboue, Debora Fernandes na Steven Mukwala.
Nyota hao wamechukua nafasi za Moussa Camara, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’, Che Fondoh Malone, Fabrice Ngoma na Leonel Ateba.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Ally Salim (1), David Kameta (3), Valentin Nouma (29), Karaboue Chamou (2), Abdurazak Hamza (14), Yusuph Kagoma (21), Kibu Denis (38), Debora Fernandes (17), Steven Mukwala (11), Jean Charles Ahoua (10), Elie Mpanzu (34).
Wachezaji wa Akiba
Hussein Abel (30), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Fabrice Ngoma (6), Joshua Mutale (7), Ladaki Chasambi (36), Awesu Awesu (23), Leonel Ateba (13), Valentino Mashaka (27). Alexander Erasto (42).